Posts

Showing posts from October, 2023

RAIS MWINYI AVITAKA VIKOSI VYA SMZ KUENDELEZA UADILIFU

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amevinasihi vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza uadilifu na uwajibikaji wa majukumu yao ya kila siku. Dk. Mwinyi ambae ni Kamanda Mkuu wa Idara Maalum ya vikosi vya SMZ, alitoa nasaha hizo viwanja vya JKU – Kama, alipozungumza na wapiganaji kwa lengo la kuwapongeza kutokana na juhudi zao za kuhakikisha amani na utulivu nchini vinaendelea kuimarishwa. Alivitaka vikosi hivyo kuweka mbele maslahi ya nchi kwanza, uwajibikaji pamoja na kusimamia uadilifu jeshini. Rais Dk. Mwinyi alivisisitiza vikosi hivyo juu ya suala zima la kusimamia nidhamu kwenye maeneo yao ya kazi ili kufanya kazi zao kwa uadilifu. “Jeshi ni nidhamu ikikosekana nidhamu katika jeshi basi hapo hakuna jeshi” alikazia Rais Dk. Mwinyi. Dk. Mwinyi pia, alivipongeza vikosi hivyo kwa jitihada zao za kutoa huduma bora kwa jamii wakiwemo Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) kupitia hospitali yao iliopo Bububu pamoja na hospitali ...